Main Menu

Saturday, December 21, 2013

MAMIA WAJITOKEZA KUMZIKA ALIYEKUWA KATIBU WA CCM MKOA WA IRINGA, NCHEMBA AONGOZA MAZISHI YAKE, RAMBIRAMBI YA LOWASSA WAZUA NGUZO

 Vijana  wa  UVCCM mkoa  wa Iringa na Mbeya  wakiwa  wamelibeba  jeneza  lenye  mwili wa aliyekuwa katibu wa CCM mkoa wa Iringa Emanuel Mteming'ombe  wakati  wa kuelekea  kanisani kwa ibada kabla ya mazishi yake  yaliyofanyika kijijini Kwo Rujewa Mbarali mkoani Mbeya
Mkuu  wa mkoa  wa Mbeya  Abas Kandoro wa pili  kushoto akiwa na mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma katikati
Mwenyekiti  wa CCM mkoa  wa Iringa Jesca Msambatavangu  akisoma historia ya marehemu Mteming'ombe huku naibu katibu mkuu  CCM Bara mwigulu Nchemba akionyesha kufuta machozi
Mjane  wa Mteming'ombe akiweka maua
Mzee Mteming'ombe akiweka shada la maua
Naibu katibu mkuu CCM Bara  Mwigulu Nchemba  akiongoza  waombolezaji kuweka shaba la maua  katika kaburi la aliyekuwa katibu wa CCM mkoa wa Iringa marehemu Emanuel Mteming'ombe katika makaburi ya RC Rujewa Mbarali Mbeya
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu  akiweka shada la maua
mkuu  wa  mkoa wa Iringa Dr Ishengoma  akiweka  shada la maua
Mkuu  wa mkoa  wa Mbeya Abas  Kandoro akiweka shada la maua
Kanali Mjengwa akisalimiana na naibu katibu mkuu CCM Bara Mgulu Nchemba  leo nje ya kanisa la RC Rujewa baada ya  kukutana kwa shughuli za mazishi ya aliyekuwa katibu wa CCM mkoa  wa Iringa Emanuel Mteming'ombe


MWENYEKITI wa  Chama cha  mapinduzi (CCM) Taifa  Dr  Jakaya  Mrisho  Kikwete  ametuma  salam  za rambirambi kwa  uongozi  wa  CCM mkoa  wa  Iringa na  familia ya aliyekuwa  katibu  wa CCM mkoa  wa  Iringa Emanuel Mteming'ombe aliyefariki  duniawiki hii na kuzikwa katika mji  wa  Rujewa Mbarali  mkoani Mbeya.

Salam  hizo  za Rais Dr  Kikwete  zilitolewa  jana   wakati  wa mazishi  ya Mteming'ombe  na naibu  katibu mkuu  CCM Bara   Mwingulu Nchemba  ambae alikiwakilisha  chama taifa  katika mazishi hayo .

Amesema  kuwa Rais Dr  Kikwete  ambaye  yupo  nchini Marekani kwa ziara  ya  kazi amepokea  kwa masikitiko makubwa  taarifa  ya  kifo  cha katibu  huyo na kuwa alitamani  sana  kuweza kufika Rujewa mkoani Mbeya  kwa ajili ya  kushirikia mazishi  hayo ila ameshindwa .


Kwa  upande  wake  mkuu wa mkoa  wa  Iringa Dr Christine Ishengoma akitoa  salama za  serikali mkoa  wa Iringa  kufuatia  kifo  hicho amesema  kuwa katika  kipindi  hiki cha maombolezo  na  baada ya maombolezo  viongozi wa chama na  serikali mkoa  wa Iringa  hawana budi kuendelea  kufanya kazi kwa  kushirikiana  zaidi kama njia ya  kumuenzi Mteming'ombe.

Huku  mkuu  wa  mkoa  wa Mbeya Abas  Kandoro akisisitiza viongozi  wa umma na chama  kujenga  utamaduni  wa kushirikiana na kuacha  tabia ya kujitenga na jamii.

Wakati  huo  huo waombolezaji  waliofurika makaburini hapo walionyesha  kushindwa  kujizuia kushangilia kwa  furaha  kubwa wakati mwenyekiti  wa CCM mkoa  wa Iringa Jesca  Msambatavangu  akisoma mchango wa  waziri mkuu aliyejiuzulu Edward Lowasa mchango  wa Tsh milioni 1  alioutuma kwa uongozi  wa CCM mkoa wa Iringa kwa ajili ya shughuli  za mazishi  ya  Kiongozi  huyo.
 
kutoka mzee wa matukio daima

0 comments:

Post a Comment