BONDIA Fransic Miyeyusho wa Tanzania amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi katika mchezo wake dhidi ya David Chalanga kutoka Kenya utakaofanyika Desemba 31 katika kwenye ukumbi wa Msasani Klabu,mchezo huo wa kufunga mwaka na kufungua mwaka utakuwa wa raundi nane.
Itakuwa chachu kwa mabondia hao wanaotamba Afrika Mashariki kugombea mikanda mikubwa ya ubingwa na kujiongezea rekodi ya ushindi wa mpambano huo unaosubiliwa kwa hamu na mashabiki wa mchezo wa masumbwi kila kona ya tanzania.
akizungumzia mpambano huo miyeyusho amesema yeye yupo fiti wakati wowote ule
kama mpinzani wake yuko tayali yeye yupo kwa ajili ya kupigana katika mpambano huo.
Katika mpambano huo,kutakuwa na Mapambano ya Utangulizi kati ya bondia Iddy Mnyeke atakaeoneshana ubabe na Cosmasi Cheka,Antony Mathias akizipiga na Fadhili Majiha Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akizichapa na Mohamed Kashinde.
0 comments:
Post a Comment