Nafasi na wakati wa klabu kama simba, hahahaha kwenye upeo wa hali ya juu
mzee wangu Shafi Adam Shafi aliandika kitabu kinachoitwa vuta n'kuvute
dhamira kubwa ni ukale na usasa.
Wakoloni walikuwa wanapinga usasa ili
waendelee kutawala wakati wazawa walivuta kwenye usasa ili wapate uhuru
lakini Shafi adam shafi alimtumia mwanaharakati aitwae Denge kuleta
suluhu kwenye jamii ile, simba wanangoja nn?
Inamaana hakuna watu kama denge? Tatizo la Simba sio Rage na solution
sio Kaburu wala Kinesi kwani na wao sio beatiful kwa hili kama
alivyosema mwandishi mmoja wa ghana anaitwa aikwey yamah'' kwenye
beatiful ones are not yet born, suluhu ya simba ni katiba mpya
itakayoifanya klabu ile iendeshwe kibiashara kwa mfumo wa kampuni.
Fikra za baraza la kina mzee hamisi kilomoni haziwezi kwenda na kasi ya
maisha ya sasa, ifikie mahala tuondokane na ukale tuliorithi kwa
wakoloni tuachane na mabaraza ya wazee tuachane na baraza la wadhamini
hayana maana twende kwenye usasa utaoifanya simba ipige hatua.
Simba
inahitaji kuwa na rais ambaye anapatikana kwa kumiliki hisa nyingi na
si busara za baraza la wazee au wanachama waliohongwa kwenda kumpigia
kura jamaa flani.
Simba inahitaji wakurugenzi wataoweza kwenda kasi na
changamoto za maisha ya kisasa, mimi sio mshabiki wala mnazi wa vilabu
vikubwa vya hapa nchini lakini mimi nimuumini wa maendeleo nimepata
fikra kama denge alivyokuwa suluhisho la kuwatoa watawala wa kikoloni
walikuwa wanaamini ukale lakini hawakuangalia nafasi ya wakati simba
inahitaji mabadiliko ina miaka 77 lakini asset kubwa mpaka leo ni
wanachama wahongwaji wanaothaminiwa wakati wa vikao tu.
Majengo mawili
ambayo ni posho za kuwalinda wazee wa klabu, timu haina uwanja hata
wenye hadhi kama ule unaotumiwa kwenye shule za msingi za tz bado
mnasema mnataka flani awe mwenyekiti hamuoni kama mnahitaji mabadiliko
mazima ya mfumo mzima wa kiuongozi.
Wacha nikaoge nijiandae na merside
derby kwani kule kunawatu wanaojitambua.
NA Issa maeda wa ebony fm
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment