Main Menu

Thursday, November 28, 2013

TASWIRA YA MUONEKANO WA TERMINAL III YA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE UTAPOKAMILIKA


Mnamo April 18, mwaka huu mamlaka ya viwanja vya ndege (TAA) ilisaini mkataba wa dola za kimarekani 168 (takriban bilioni 275 za Kitanzania) na kampuni ya BAM International ya Uholanzi kwa ajili ya ujenzi wa awamu ya kwanza ya Terminal III ya uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. 

Ujenzi wa awamu hiyo ya kwanza unaotarajiwa kuanza karibuni ukikamilika terminal hiyo itakuwa na uwezo wa kuhudumua abiria milioni 3.5, ambapo awamu yake ya pili ikikamilika itakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni 6, na itakuwa ni kwa huduma ya ndege za kimataifa. Sehemu iliyopo sasa ya uwanja huo, yaani terminal II, itatumika kwa abiria wa ndani. 




0 comments:

Post a Comment