Main Menu

Thursday, August 1, 2013

LHRC NA TLC WAMSHTAKI WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA

Kituo cha sheria na haki za binadamu kwa kushirikiana na chama cha wanasheria Tanganyika  kimewasilisha mahakama kuu jijini Dar-es-Salaam,shauri la mashtaka dhidi ya waziri mkuu wa jamuhuri ya mungano wa Tanzania ,Mheshmiwa Mizengo Pinda na mwanasheria mkuu wa serikali Mheshimiwa jaji  Fredrick Werema.
 
Wakiwasilisha shauri hilo mahakama kuu jijini Dar-es-Salaam, jopo la mawakili mbalimbali kutoka kituo cha sheria na haki za binadamum,pamoja na baadhi ya mawakili kutoka chama cha wanasheria Tanganyika na baadhi ya wanainchi.
 
 
Wakiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuwasilisha hati ya mashtaka,mjumbe wa bodi ya kituo cha sheria na haki za biandamu Dr Ringo Tenga,amesema wanaangali matamshi yanayo hatarisha haki za biandamu lazima mambo hayo wayafikishe mahakamani.
 
Katika hatua nyingine mwakilishi wa taasisi ya kufuatilia na kuangalia shughuli na mwenendo wa bunge kwa niaba ya wananchi bwana Marccosy Albanie amesema kuwa,wanaandaa mashtaka mengine dhidi ya waziri mkuu kwenda kwa wanainchi,kufuatia kauli yake kuwa serikali imechoka na hakuna namna nyingine ili wanainchi nao waamue.
 
Shitaka hilo litakalo kuwa chini ya mawakili 20,ambapo baada ya kuwasilishwa mahakamani, kitakachofuata ni kupangwa kwa tarehe ya kuanza kusikilizwa kwa shauri hilo, pamoja na jaji atakaye lisikiliza ikiwa ni pamoja na watuhumiwa wa shitaka hilo kupelekewa walaka wa kuitwa mahakamini ili kujibu mashtaka yanayo wakabili.
 
Shitaka hilo namba 24 la mwaka 2013 dhidi ya waziri mkuu wa jamuhuri ya mungano wa Tanzania mheshimiwa Mizengo na mwanasheria mkuu wa serikali mheshimiwa jaji mstaafu Fredrick Welema, linafuatia kauli ya waziri mkuu aliyoitoa bungeni mjini Dodoma kwenye kikao cha tarehe 20 mwezi wa sita 2013, akiwaamuru polisi kuwapiga wale wote watakao kaidi kutii amri halali za jeshi la polisi kuwa watapigwa.

0 comments:

Post a Comment