Timu
ya Taifa ya Uganda (The Cranes) imewasili Dar es Salaam leo tayari kwa
mechi ya kwanza ya mchujo kusaka tiketi ya Fainali za Afrika kwa
Wachezaji wa Ligi ya Ndani (CHAN) kati yake na Tanzania (Taifa Stars)
itakayochezwa Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
The
Cranes inayofundishwa na Mserbia Sredojvic Micho imetua Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 5.30 asubuhi kwa ndege ya Air
Uganda, na imefikia hoteli ya Sapphire.
Timu
hiyo leo (Julai 11 mwaka huu) itafanya mazoezi saa 9 alasiri kwenye
Uwanja wa Karume, wakati kesho saa 9 alasiri itafanya mazoezi Uwanja wa
Taifa, kabla ya kuipisha Taifa Stars itakayoanza mazoezi saa 10 kamili
jioni.
Taifa
Stars inayofundishwa na Mdenmark Kim Poulsen, na kudhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager, leo kwa mujibu wa program yake haitakuwa na
mazoezi.
Wachezaji
wanaounda The Cranes ni makipa Ismail Watenga, Kimera Ali na Muwonge
Hamza. Mabeki ni Guma Dennis, Kasaaga Richard, Kawooya Fahad, Kisalita
Ayub, Magombe Hakim, Malinga Richard, Mukisa Yusuf, Savio Kabugo na
Wadada Nicholas.
Viungo
ni Ali Feni, Birungi Michael, Frank Kalanda, Hassan Wasswa, Kyeyune
Said, Majwega Brian, Mpande Joseph, Muganga Ronald, Ntege Ivan, Owen
Kasule, wakati washambuliaji ni Edema Patrick, Herman Wasswa na Tonny
Odur.
TENGA KUZUNGUMZA NA WAANDISHI KESHO
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga atakuwa
na mkutano na waandishi wa habari. Mkutano huo utafanyika kesho (Julai
12 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwenye hoteli ya Tansoma.
Kutokana
na mkutano huo, sasa mkutano kati ya makocha wa Taifa Stars na The
Cranes uliokuwa ufanyike saa 5 asubuhi ofisi za TFF nao umehamishiwa
hoteli ya Tansoma. Mkutano huo pia utahusisha manahodha wa timu zote
mbili.
WAJUMBE MKUTANO MKUU MAALUMU KUWASILI KESHO
Wajumbe
wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
utakaofanyika Jumamosi (Julai 13 mwaka huu) wanawasili jijini Dar es
Salaam kesho (Julai 12 mwaka huu).
Mkutano
huo wa marekebisho ya Katiba utakuwa chini ya uenyekiti wa Rais wa TFF,
Leodegar Tenga na utafanyika ukumbi wa NSSF Waterfront kuanzia saa 3
kamili asubuhi. Wajumbe wote wa mkutano huo watafikia hoteli ya
Travertine.
Pia
mkutano huo utahudhuriwa na wageni mbalimbali waalikwa wakiwemo kutoka
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na Chama cha Mpira wa
Miguu Zanzibar (ZFA).
MECHI YA STAND, KIMONDO NAYO KUPIGWA JUMAPILI
Mechi
ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) kati ya Stand United FC
ya Shinyanga na Kimondo SC ya Mbeya iliyokuwa ichezwe Jumamosi (Julai
13 mwaka huu) imesogezwa mbele kwa siku moja.
Timu
hizo sasa zitacheza Jumapili (Julai 14 mwaka huu) kwenye Uwanja wa
Kambarage mjini Shinyanga. Kimondo ilishinda bao 1-0 mechi ya kwanza
iliyochezwa Julai 6 mwaka huu Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini
Mbeya.
Mechi
nyingine ya ligi hiyo itakuwa kati ya Friends Rangers ya Dar es Salaam
na Polisi Jamii ya Mara, na itafanyika kwenye Uwanja wa Azam ulioko
Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Mwamuzi wa mechi hiyo ni
Hans Mabena kutoka Tanga.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment