Mmoja
wa wafanyakazi wa Kampuni ya Jambo Freight Forwarder Bibi Vanessa Gwau
kushoto akielezea jambo kwa mwandishi wa habari wakati wa hafla ya
kupokea mabomba yatakayotumika kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadio Dar
es Salaam. Jambo Freight ndiyo kampuni iliyopewa zabuni ya kupakua
shehena hiyo.
Balozi
wa Jamhuri ya Watu wa China Balozi Lu Youging katikati akifafanua
jambo,kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Prosefa Sospeter
Muhongo,kutoka kulia Ms Wang Fang kutota Ubalozi wa China anayemfuatia
ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Sadick Meck Sadick.
Waziri
Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda akiwasili katika eneo la Bandari ya Dar
es Salaam tayari kwa kuzindua rasmi upokeaji wa shehena ya mabomba
yatakayotumika katika ujenzi wa mradi wa kusafirisha Gesi kutoka Mtwara
hadi Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda katika akibadishana jambo na Waziri wa
Nishati na Madini Prosefa Sospeter Muhongo aliyekaa kushoto,Kulia ni
Balozi wa China nchini Tanzania
Balozi Lu Youging wakati wa hafla ya kuzindua kupokea shehena ya mabomba
kwa ajili ya mradi wa kusafirisha Gesi kutoka Mtwara hadi Dar es
Salaam.
Waziri
Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda akishuhudia Balozi wa Jamhuri ya Watu wa
China Balozi Lu Youging alipokuwa akimalizia kufunua kitamba kama ishara
ya uzinduzi rasmi wa upakeaji wa mabomba ya Gesi.
Pichani mafundi wakiwa katika zoezi la kupakua mabomba kutoka katika meli na kupakia kwenye Lori tayari kwa safari ya Mtwara.
Waziri
Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda akizungumza mara baada ya kuzindua rasmi
upokeaji wa mabomba ya gesi tayari kwa kusafishwa hadi Mtwara.
PICHA ZOTE NA FRANK SHIJA - MAELEZO
Serikali imewatoa hofu wananchi wa Mtwara kuhusu kunufaika kwao na gesi asilia iliyopatikana katika maeneo yao.
Hayo
yamebainishwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo
Pinda alipokuwa akizindua rasmi upokeaji wa shehena ya mabonba ya gezi
kwa ajili ya mradi wa bomba la kusafirishia Gesi kutoka Mtwara hadi Dar
es Salaam mwisho ni wiki jijini Dare se Salaam.
Pinda
amesema kuwa wananchi wa watanzania watanufainaka na mradi huo hasa
hasa wakazi wa Mtwara kwakuwa vijana wengi watapata ajira wakati na
baada ya kukamilika kwa ujenzi wa bomba hilo kwakuwa viwanda mbalimbali
vitajengwa mkoani Mtwara kikiwemo kiwanda cha Saruji ambacho ujenzi wake
umekwisha anza.
“Ndugu
zangu wana Mtwara ni waambe tu wakati wa kunufaina na rasilimali ya
Gesi sasa umefika,niseme tu mradi huu utakapokamilika fursa mbalimbali
zitafunguka ikiwemo ajira kwa wakazi wa Mtwara”. Alisema Pinda.
Kwa
upande wake Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Chini hapa nchini Balozi Lu
Youging amesema kuwa Tanzania itanufaika na mradi huu na kukua kiuchumi
kwakuwa itapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi katika nishati na badala
yake itazalisha nishati yakutosha.
Balozi
huyo aliongeza kuwa kutpitia mradi huu Tanzania itaondokana na kuwa
tegemezi katika shughuli zake za maendeleo kwa kuwa kuna hazina ya
kutosha ya gesi asilia na itawanufaisha watanzania wenyewe na si
vinginevyo.
Jumla
ya mabomba 3400 yamepokelewa katika awamu ya kwanza ambapo awamu ya
pili itapokelewa shehena yenye mabonmba 4600 katika bandari ya
Mtwara.Inakadiriwa kuwa jumla ya shehena 12 zitatumika mpaka mradi
utakapokuwa umekamilika.
0 comments:
Post a Comment