Wakala wa mshambulizi matata wa Liverpool, Luis
Suarez, amefanya mazungumzo na kocha wa klabu hiyo Brendan Rodgers na
mkurugenzi mkuu
Ian Ayre na kukariri kuwa mchezaji huyo kutoka Uruguay,
angali ana nia kubwa ya kushiriki katika michuano ya kuwania kombe la
klabu bingwa barani Ulaya msimu ujao.
Suarez, kwa sasa yuko likizoni, baada ya kuichezea timu ya taifa ya Uruguay, wakati wa michuano ya kuwania kombe la Shirikisho nchini Brazil.
Lakini katika miezi ya hivi karibu, Suarez amedokeza kuwa nia yake kuu msimu ujao ni kushiriki katika michauno ya Ulaya na inaaminika kuwa wakala wake Pere Guardiola alisasilisha ujumbe huo kwa wasimamizi wa klabuhiyo ya Liverpool hiyo jana.
Je ndoto ya Suarez itatimia?
Tayari Liverpool, imekataa ombi kutoka kwa klabu ya Arsenal ya kutaka kumsajili mchezaji huyo kwa kitita cha pauni milioni thelathini, licha ya kuwa mchezaji huyo ameelezea wazi wazi kutoridhishwa kwake na maisha ya Uingereza.Suarez anatumikia adhabu ya kutoshiriki katika mechi kumi baada ya kupatikana na hatia ya kumuuma mchezaji wa Chelsea, Branislav Ivanovic wakati wa mechi yao katika uwanja wa Anfeld msimu uliopita na katika siku za hivi karibuni amekuwa akihusishwa na klabu ya Real Madrid.
Ripoti zinasema huenda Liverpool, ikakubali ombi kutoka kwa klabu ambayo itakuwa tayari kulipia takriban pauni milioni hamsini, sawa na kiasi ambacho Chelsea kililipa wakati ilipomsajili Fernando Torres Janauri mwaka wa 2011.
Msimu uliopita, Suarez alishutumiwa sana, kutokana na kile wakosoaji wake walitaja kuwa mtindo wa kujiangusha ili kupata mkwaju wa adhabu
Chanzo bbcswahili
0 comments:
Post a Comment