Barcelona imemtangaza Argentine Gerardo Martino Tata kuwa
kocha mpya wa wa klabu hiyo kwa mkataba
wa miaka miwili kuchukua nafasi ya meneja iliyoachwa wazi na Tito Vilavano
aliyeachia ngazi.
Gerardo Martino
mwenye umri wa miaka 50 alichukua taji la ligi kuu ya Argentina msimu uliopita
maarufu Clausura akiwa na klabu ya Newell's Old Boys amekaa nje ya masuala ya soka miezi
sita.
Gerardo
Matinho kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Paraguay anakuwa kocha wa nne
kutoka nchi ya Argentina kuifundisha Barcelona wengine Helenio Herrera, Roque Olsen na Cesar Luis Menotti.
Muargentina
huyo anayesifika kufundisha mpira wa kuvutia amewazidi makocha Luis
Enrique, Andre Villas-Boas, Michael Laudrup, Marcelona
Bielsa na Guus Hiddink aliyeacha kazi kwenye klabu ya Anzhi Makhachkala.
Wachezaji wa Barcelona, wakiwemo Carles
Puyol, Messi na kipa Jose Manuel Pinto walihudhuria mkutano wa kujiuzulu
kwa Vilanova ulioongozwa na Rais, Sandro Rosell
MJUE GERARDO MARTINO
1962: Alizaliwa Novemba 20 mjini Rosario, Argentina.
1980-90: Kiungo
huyo mshambuliaji anajiunga na Newell Old Boys ya Argentina na
kuichezea mechi 392 za ligi, akifunga mabao 35 ndani ya miaka 10.
Alitwaa taji la Primera Division mwaka 1988.
1991: Alicheza mwaka mmoja Tenerife na kuichezea mechi moja timu ya taifa yaArgentina chini ya Alfio Basile.
1991-94: Alirejea Newell Old Boys kwa miaka mitatu na kutwaa mataji mawili zaidi ya Argentina.
1994-95: Aliichezea kwa msimu mmoja Lanus kabla ya kurejea Newell Old Boys.
1996: Alikwenda Ecuadorian kuichezea mwaka mmoja Barcelona Sporting Club na kisha O'Higgins ya Chile.
1998: Alifanya kazi ya ukocha kwa mara ya kwanza Brown de Arrecifes.
1999: Alijiunga na Platense kama kocha.
2000: Alikuwa kocha Mkuu wa Instituto.
2002-03: Aliiongoza Libertad kutwaa mataji mawili ya Paraguay.
2004: Alitwaa taji la Paraguay akiwa na Cerro Porteno.
2005: Alikuwa kocha wa Colon kwa msimu.
2005-06: Alirejea Libertad na kutwaa taji la nne la Paraguay mwaka 2006.
2007: Februari - alikuwa kocha wa timu ya taifa ya Paraguay na akashinda tuzo ya Kocha bora wa Mwaka Amerika Kusini.
2010: Juni - Aliiongoza Paraguay katika Kombe la Dunia Afrika Kusini na kuifikisha hadi Robo Fainali, ambako ilifungwa na Hispania.
2011: Baada ya Paraguay kufungwa katika Fainali ya Copa America na Uruguay, ajajiuzulu ukocha wa timu hiyo ya taifa.
2012-13: Alirejea Newell Old Boys kama kocha na kutwaa taji la Clausura mwaka 2013.
2013: Julai 23 - Anakubali Mkataba wa miaka miwili Barcelona, kurithi mikoba ya Tito Vilanova.
0 comments:
Post a Comment