Main Menu

Friday, June 21, 2013

WATU WAWILI WATIWA MBARONI KWA KUMDUNDA MBUNGE WA KASULU MJINI MOSES MACHAL


Jeshi la Polisi Mkoa Dodoma linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kumvamia na kumshambulia Mheshimiwa MOSES S/O MACHALI, miaka 31, Muha, Mbunge wa Kasulu Mjini kupitia NCCR – Mageuzi wakati anaelekea nyumbani kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Bw. David. A. Misime alisema Tukio hilo limetokea tarehe 20/06/2013 majira ya 19.00 hrs katika eneo la Area ‘E’ katika Manispaa ya Dodoma.

“alikutana na vijana wanne (4) walikouwa amesimama katikati ya barabara akapiga honi lakini hawakupisha. Aliamua kuwauliza “Jamani mnasimama katikati ya barabara si nitawagonga?” Nao wakamjibu: “Wewe si unajifanya mtto wa Mbunge, tutakupiga sasa”. Alisisitiza Kamanda Misime.

Kamanda Misime alisema Mheshimiwa alipojaribu kupita vijana hao walipiga gari lake. kitu ambacho kilimfanya ashuke ili atazame kama gari hilo limepata uharibifu.wowote, ndipo vijana hao wakaanza kumshambulia kwa ngumi na mateke huku naye akijitahidi kujihami.

Hata hivyo Bw.Misime alisema, walitokea vijana wawili (2) na kumsaidia. Mheshimiwa mbunge ambapo kijana mmoja kati ya waliokuwa wanamshambulia Mheshimiwa Machali ‘alimng’ata’ mgongoni kijana aliyekuwa anamsaidia Mheshimiwa Mbunge.

Bw. Misime alisema Watuhumiwa baada ya kuona wamezidiwa nguvu walitimua mbio. Ambapo pia Mheshimiwa Machali aligundua kuwa simu yake ya mkononi wameondoka nayo vijana hao.

Kamanda David. A. Misime alisema jeshi la Polisi mkoani Dodoma lilifanya Msako mkali ulifanyika usiku wa manane ambapo watuhumiwa wawili (2) walikamatwa ambao aliwataja kuwa ni JEREMIA LAWRENT MKUDE@ JERRY, Miaka 18, Mkaguru Mkazi wa Chaduru, Manispaa ya Dodoma. aliyekutwa akiwa na jeraha usoni alilopata wakati anapambana na Mheshimiwa Mbunge na vijana waliokuwa wanamsaidia.

Kamanda huyo wa Polisi Mkoa wa Dododoma alimtaja mtuhumiwa mwingine anayeshikiliwa na jeshi la polisi kuwa ni CHARLES CHIKUMBILI, Miaka 22, Mkulima, Mkazi wa Swaswa, katika Manispaa ya Dodoma.

Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Bw. David Misime alisema askari walipowafanyia upekuzi wa mwili watuhumiwa usiku huo wa manane wamekutwa na misokoto miwili (2) ya bhangi.

Na. Jeshi la Polisi Dodoma.


0 comments:

Post a Comment