Idara ya Ujasusi ya Marekani imeweka bayana kwamba
inajitegemea kwa ulinzi katika ziara nzima ya Rais Barack Obama kwa nchi
za Afrika, ikiwemo Tanzania, Afrika Kusini na Senegal.
Kwa mujibu wa taarifa ya idara hiyo, katika kuhakikisha usalama wa
kutosha wakati wa ziara ya Obama tayari maofisa wao wameshakamilisha
maandalizi ya kiusalama katika nchi zote anazotarajiwa kutembelea.
Meli ya kivita kutua bandarini
Katika kuchukua hatua hizo, meli kubwa kabisa ya kivita yenye hospitali
maalum zipo tayari kwa ya kambi maalumu katika bandari maalum za nchi
atakazotembelea, kwa ajili ya kukabiliana na dharura yoyote ya kiafya ya
Obama na familia yake.
Ili kuwawezesha maofisa wa kijasusi wa Marekani, ndege ya kijeshi ndiyo
itakayobeba magari 56 zikiwemo limousine 14 na magari matatu maalumu ya
kubeba mizigo.
Malori hayo yatakuwa yakibeba vioo ambavyo ni vizuizi maalumu vya risasi
na milipuko kwa ajili ya kuongeza ulinzi kwenye hoteli atakazolala yeye
na familia yake.
Ndege za kivita kutawala anga
Ndege za kivita zitakuwa zikiruka kwa zamu wakati wote muda wa sasa 24
kwa ajili ya kuhakikisha ulinzi katika sehemu atakayokuwa Rais Obama na
kudhibiti anga yote kwa wakati huo dhidi ya ndege yoyote ngeni
itakatosogea usawa wao.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Mwananchi, hakuna Maandalizi ya
safari hiyo ambayo tayari yamekamilika yanapolinganishwa na safari
nyingine za aina hiyo zilizowahi kufanyika, waraka maalumu kuhusu suala
la usalama unaonesha kwamba kumekuwa na juhudi za ziada zakuhakikisha
ulinzi wa Amiri jeshi huyo Mkuu wa Marekani akiwa nje ya nchi.
Kabla ya safari yake kwa nchi za Afrika, Obama atatembelea Ireland na
Ujerumani ikiwa ni sehemu ya kuongeza changamoto inayokabili masuala ya
usalama wake.
Lakini zaidi, safari ya Obama kwa nchi za Afrika inadhaniwa kuwa
inayolazimisha waandaaji kuwa na umakini wa hali ya juu na kuifanya iwe
aghali zaidi katika utawala wa Obama kuliko ziara katika nchi za ulaya,
kwa mujibu wa wataalamu wa mipango.
Familia ya rais huyo inatarajiwa kutembelea nchi tatu za Afrika, ikiwemo
Tanzania, Afrika Kusini na Senagal kuanzia Juni 26 hadi Julai 3 mwaka
huu.
Serikali ya Marekani inahakikisha kwamba inasimamia kwa silimia 100
ulinzi wa familia hiyo inapokuwa nje ya nchi na haihitaji kutumia vyombo
vya usalama vya nchi husika ikiwemo polisi, majeshi, na huduma za
hospitali.
Safari yaahirishwa
Katika ziara ya Obama nchini Tanzania, safari ya kutembelea Mbuga ya
Wanyama ya Mikumi yeye pamoja na familia yake imeahirishwa ili kupunguza
ukubwa wa gharama katika safari yake.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa juzi, Obama hatatembelea tena mbuga za
wanyama kama ilivyopangwa awali, bali imependekezwa kwamba sehemu
atakayoweza kufika ni katika Gereza la Visiwa vya Roben nchini Afrika
Kusini ambako Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, kuahirishwa kwa safari ya mbugani kunatokana
na gharama kubwa inayohitajika kwa ajili ya kupata walinzi maalumu
wakiwemo wadunguaji wenye silaha nzito ambao watakabiliana na wanyama
wakali.
Safari hii ya Obama nje ya nchi zinafanyika wakati wakala wa Serikali
ikiwemo Idara Maalumu ya Ujasusi zikichuana kuhusu namna ya kupunguza
matumizi.
Idara hiyo inalazimika kupunguza kiasi cha Dola 84 milioni (Sh134.2
bilioni) mwaka huu na hiyo inailazimisha kufuta safari ya kitalii ya
Ikulu ya Marekani ambayo itasaidia kuokoa Dola 74,000 (Sh118.2 milioni )
kama posho ya muda wa ziada wa kazi kwa wiki kwa kila askari.
Gharama za safari hii
Safari ya sasa ya Obama itagharimu serikali kuu kati ya Dola 60 milioni
hadi Dola 100 milioni (Sh 159.2 bilioni), kwa makadirio ya safari za
aina hiyo zilizofanyika kwa mataifa ya Afrika miaka ya hivi karibuni.
Makadirio hayo yamefanywa na mmoja wa wataalamu wenye uzoefu na safari
hizo ambaye hakutaka kutajwa jina lake kwa kuwa si msemaji rasmi.
Mwananchi
0 comments:
Post a Comment