Main Menu

Wednesday, June 26, 2013

KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU CHAMJIA JUU WAZIRI MKUU NA KAULI ZAKE ZA UTATA


Kituo cha sheria na haki za binadamu nchini LHRC kwa kushirikiana na watu zaidi ya 1,000 kutoka sehemu mbalimbali nchini wamemjia juu waziri Mkuu Mizengo Pinda kutokana na kauli yake aliyoitoa bungeni hivi karibuni ya kuwapa kibali polisi kupiga raia wanaonekana hawatii amri ya jeshi hilo.

Mkurugenzi wa kituo hicho Hellen Kijo- Bisimba amesema kutokana na kusikitishwa na kauli hiyo wameamua kuandaa waraka unaokusanya saini za watanzania zikimtaka waziri Mkuu afute kauli yake na kuwaomba radhi watanzania.

Bisimba amewaeleza wandishi wa habari jijini Dar es salaam jana kuwa kauli hiyo aliyoitoa waziri Mkuu inapingana na sheria namba 6 (b) ambayo inazuia mtu kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka atakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo.

Ameongeza kuwa ni kinyume na kifungu namba 21 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai inayounda sura namba 20 ya sheria za Tanzania inayozuia matumizi ya nguvu kupita kiasi na kifungu namba 46 cha sheria ya jeshi la polisi ambayo inaelekeza kukamatwa kwa mtu aliyetenda kosa na sio kupigwa.


Bisimba ametumia mkutano huo na wandishi wa habari kumkumbusha waziri mkuu kuwa utawala wa sheria unajumuisha serikali na vyombo vya utekelezaji na ulinzi pamoja na wananchi kuheshimu sheria na kuongeza kuwa tamko lake linatoa mwanya na nguvu kubwa kwa vyombo vya usimamizi wa sheria kuvunja haki za raia.

Alipotakiwa kutoa mtizamo wake kutokana na kauli hizi zenye utata kwamba hii ni mara ya tatu kwa waziri Mkuu tangu aingia madarakani kutoa kauli ambazo zimekuwa zikiwaacha watu njia panda, kama ile ya liwalo na liwe kesho yake akatekwa ulimboka.


0 comments:

Post a Comment