Kocha Jose Mourinho amerejea katika klabu yake ya
zamani ya Chelsea leo, huku akijiita 'Mwenye furaha'
badala ya sifa yake iliyozoeleka ya 'Mtu Maalumu.'
Huku
kukiwa na waandishi wa habari karibu 250 kutoka ndani na
nje ya Uingereza, na vituo kadhaa vya televisheni
vikisongamana katika chumba alikofikia katika uwanja wa
Stamfort Bridge, mkufunzi huyo kutoka Ureno, alionekana
mwenye kuendelea kuwa na mvuto kwa vyombo vya habari.
Mourinho amewaambia waandishi wa habari kwamba
angekuwa mwenye kuchagua jina la utani, basi
angechagua jina la 'mwenye furaha.'
Mourinho aliyeifundisha Chelsea hapo kabla anarudi
akitokea Real Madrid ya Uhispania.
Monday, June 10, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment