Main Menu

Thursday, June 27, 2013

ITALY KULIPIZA KISASI KWA SPAIN LEO? KOMBE LA MABARA.


Katika mechi za Kombe la Mabara - Confederations Cup, Uhispania wanachuwana leo na Italia katika nusu fainali ya pili ya kumtafuta mshindi atakayekutana na Brazil katika fainali. 

Wenyeji Brazil waliwamwaga Uruguay mabao mawili kwa moja katika nusu fainali ya kwanza iliyochezwa jana mjini Belo Horizonte. 


Wengi wanaiona mechi kati ya Uhispania na Italia kuwa ni marudio ya fainali ya kombe la mataifa ya Ulaya - UEFA EURO mwaka wa 2012, ambapo Uhispania iliwamiminia Italia magoli manne kwa sifuri. 

Uruguay itachuwana na atakayeshindwa katika mechi ya leo, ili kumtafuta mshindi wa nafasi ya tatu.

0 comments:

Post a Comment