Wednesday, June 19, 2013
ALGERIA YAJIONDOA KATIKA MICHUANO YA KUFUZU KWA FAINALI ZA CHAN 2014 AFRIKA YA KUSINI.
Shirikisho la soka nchini Algeria imetangaza kujiondoa katika kushishiriki michuano ya kufuzu kwa fainali ya CHAN mwakani zitakazofanyika nchini Afrika ya kusini.
Taarifa kutoka ndani ya shirikisho hilo zimearifu kuwa sababu ya kujiondoa katika ushiriki wa mashindano hayo ambao hushirikisha wachezaji wanaocheza ndani ya nchi ni kushindwa kupata kikosi cha ushindani kwenye michuano hiyo.
Pamoja na baadhi ya vyombo vya habari kueleza kuwa sababu ya taifa hilo kujiondoa katika mashindano ni kuhofia halia ya usalama kwenye nchini walizopangiwa kucheza nazo ikiwemo Libya na hofu ya kuporomoka zaidi kisoka, FA ya Algeria imekanusha uvumi huo.
Algeria inashika nafasi ya 35 katika ubora wa soka duniani kwamujibu wa takwimu zilizotolewa na shirikisho la soka duniani Fifa mwezi.
Na yusuph mkule.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment