Main Menu

Monday, April 29, 2013

JAJI MKUU WA KENYA AKANUSHA KUPOKEA HONGO ILI AMPENDELEE RAIS UHURU KENYATTA

Jaji Mkuu wa Kenya, Willy Mutunga, amekanusha madai kwamba alipokea hongo kwa lengo la kumpendelea Rais Uhuru Kenyatta, wakati wa kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Machi 4 mwaka huu.

Majaji wa Mahakama ya Juu ya Kenya wakiongozwa na Mutunga, walipitisha uamuzi kuwa Kenyatta alichaguliwa kihalali na kutupilia mbali kesi ya kupinga matokeo iliyofunguliwa na mgombea mwingine Raila Odinga.

Hata hivyo, Odinga, waziri mkuu wa zamani wa Kenya, alikubaliana na uamuzi huo wa mahakama.

Mutunga amekanusha madai hayo kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii ya Twitter na Facebook.

Amesema kama kuna mtu ana ushahidi wa yeye kupokea hongo, auwasilishe kwa tume ya idara ya mahakama.

Amesema hana wasiwasi wowote kwa sababu hajapokea hongo na kwamba kama kuna mtu yeyote angejitokeza na kumpa hongo, angemfungulia mashtaka kulingana na katiba na sheria za Kenya, bila ya kujali wadhifa
wake.

0 comments:

Post a Comment