Mahakama ya Umoja wa Ulaya nchini Kosovo, leo imewahukumu adhabu ya
hadi kifungo cha miaka minane jela, watu watano kwa tuhuma za kuuza viungo
vya binadamu isivyo halali.
Watu hao wanatuhumiwa kuuza viungo hivyo
katika zahanati ya Pristina mwaka 2008.
Miongoni mwa waliohukumiwa
adhabu hiyo ni pamoja na daktari wa magonjwa ya kiume, Lufti Dervishi.
Jaji
kiongozi katika kesi hiyo kutoka Poland, Arkadiusz Sedek amesema kuwa
watu hao watatumikia adhabu hiyo kati ya mwaka mmoja hadi miaka minane
jela.
Watuhumiwa wawili katika kesi hiyo iliyofunguliwa mwaka 2011,
wamefutiwa mashtaka na kuachiwa huru.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment