Mamilioni ya wananchi wa Venezuela wamejitokeza katika mji mkuu
wa nchi hiyo Caracas kuaga mwili wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Hugo
Chavez aliyefariki dunia siku ya Jumanne kutokana na maradhi ya kensa.
Umati mkubwa wa watu ilisindikiza mwili huo kwa zaidi ya masaa 6 hadi
kufika katika akademia ya jeshi ambako kiongozi huyo atazikwa kesho
Ijumaa.
Viongozi wa America ya Latini tayari wameshawasili mjini Caracas
kwa ajili ya kutoa heshima zao za mwisho akiwemo Rais Cristina
Fernandes de Kirchner wa Argentina, Jose Mujica wa Uruguai, Evo Morales
wa Bolivia na wengineo.
Nchi nyingi duniani zinaendelea kutuma risala zao za rambirambi na
pole kwa wananchi wa Venezuela kufuatia kifo cha rais Hugo Chavez.
Rais
Barack wa Marekani hakutoa mkono wa pole bali ametoa risala fupi akitaka
kufunguliwa ukurasa mpya kuhusiana na utajiri wa mafuta ya nchi hiyo.
Miongoni mwa masuala yatakayokumbukwa kuhusiana na kiongozi hiyo
mwanamapinduzi wa Venezuela ni kuanzisha harakati ya mrengo wa kushoto
iliyoenea katika eneo la Amerika ya Latini ya kupinga ukoloni na ubeberu
wa madola ya Magharibi hasa Marekani na kupambana na umasikini.
0 comments:
Post a Comment