Washukiwa wa kundi la kiisilamu
wamewakata vichwa watu kadhaa mjini Maiduguri, Kaskazini mwa Nigeria.
Mtu mmoja ameambia BBC kuwa wanaume
watano waliuawa wakati wa msako katika nyumba za watu usiku wa kuamkia leo.
Miongoni mwa walionyongwa ni baba na
mwanawe.
Hata hivyo, jeshi la Nigerialimesema
ni watu watatu pekee waliouawa.
Zaidi ya watu 20 sasa wamefariki
katika mashambulizi tofauti, Kaskazini mwa Nigeria wiki hii pekee ambayo
yanshukliwa kusababishwa na kundi la Boko Haram pamoja na makundi mengine
yanayotaka nchi hiyo kutumia sheria za kiisilamu.
Boko Haram wamelaumiwa kwa mauaji ya
watu 23 katika mashambulizi tofauti Kaskazini mwa Nigeria.
Walio shuhudia mauaji hayo wanasema
kuwa washambuliaji waliwalenga watu waliokuwa wanauza nyama ya wanyamapori,
katika eneo la Damboa siku ya Jumatatu na kuwaua watu 18.
Watu wengine watano walifariki
Jumanne wakati kundi la wanaume waliokuwa wanacheza mchezo wa kamari
walishambuliwa mjini Kano.
silaha zilizokamatwa katika operesheni iliyofanyika
Kundi la Boko Haram, linalopigana
kutaka kuweka sheria za kiisilamu, nchini Nigeria limekuwa likifanya
mashambulizi, katika sehemu kadhaa nchini humo.
Boko Haram imelaumiwa kwa vifo vya
takriban watu 1,400, Kaskazini mwa Nigeria tangu mwaka 2010. Mwaka jana pekee ,
kundi hilo lilihusishwa na vifo vya watu 600.
Siku ya Jumatatu, watu waliokuwa
wamejihami, walifyatulia risasi katika soko moja jimbo la Borno , wakiwalenga
watu waliokuwa wanauza nyama ya nyani, na nguruwe.
Waisilamu wengi hawatumii kabisa
nyama ya wanyama pori.
"watu waliokuwa wamejihami, na
wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi la Boko Haram, walikuja katika soko moja
eneo hilo, na kuwapiga risasi watu 13, papo hapo na wengine watano walifariki
kutokana na majereha yao.'' alisema afisaa mmoja.
Eneo la Damboa liko karibu na
hospitali moja mjini Borno katika jimbo la Maiduguri, ngome ya Boko Haram.Kundi
hilo liliundwa mjini humo mwaka 2002.
Wakati huohuo, ripoti zinasema kuwa
shambulizi lengine baya sana limefanywa mjini Kano , mji mkuu Kaskazini mwa
Nigeria,umbali wa kilomita 500, Magharibi mwa Damboa.
Watu waliokuwa wanaendesha pikipiki
waliwanywaftulia risasi, vijana waliokuwa wanacheza nje , kwa mujibu wa taarifa
za polisi.
Mchezo wa kamari pia umeharamishwa
katika dini ya kiisilamu.
CHANZO BBCSWAHILI
0 comments:
Post a Comment