Main Menu

Sunday, January 6, 2013

RAPPER MKARE KUTOKA MAGENGE YA 254 OCTOPIZZO AFUNGUKA KUHUSU TUHUMA ZA KUWA FREEMASON

Inawezekana sasa hivi baadhi watu ni kama wamechoka kusikia freemason stories, lakini ukweli ni kwamba bado zinawasumbua watu wengi hasa mastaa duniani ama wanasiasa maarufu, na ukizingatia idadi kubwa ya watu wanaonekana kuzielewa vizuri zaidi alama zinazosemekana kuwa za imani hiyo.

Msanii maarufu na mwenye mafanikio sana wa nchini Kenya na sasa Afrika inamfahamu Octopizzo amekuwa kwenye tetesi za kuwa mfuasi wa Illuminati kama inavyojulikana zaidi Kenya ama Freemason, lakini hivi karibuni ndo kawashtua zaidi watu baada ya kutoa video yake ya wimbo wa ‘Swag’ ambao umejaa ishara kadhaa zinazosemekana kuwa ni za Freemason.
Katika video hiyo kuna Pyramids zikiwa zinawaka moto zikiwa kwenye background, na pia jichoni akiwa amejichora alama ya pembe tatu na ishara nyingine nyingi, Video hiyo imeongozwa na director maarufu Enos Elik na ndani kashirikishwa msichana mzuri Amina. 

Katika interview aliyofanya na mtangazaji wa kipindi cha Mambo Mseto maarufu kwa jina la Mzazi M. Tuva, Octop aliulizwa kuhusu tuhuma hizo za u-freemason na sehemu ya maswali na majibu yao yalikuwa hivi:

Tuva: Jo! Watu wameongea.

Optopizzo: wamesema nini?

Tuva: wameongea sana, wanauliza hizo ni nini umechora kwa sura?

Octopizzo: kwani ni wapi iliwekwa official kuwa triangle ni ya Illuminati(Freemason)?

Tuva: Kwa hiyo wewe ni member au sio member?

Optopizzo: Mi ni member wa Sir God.

Hapo atakuwa ameeleweka Octoppizo, mengine labda ni yake ya moyoni.
 


kutoka leotainment tz

0 comments:

Post a Comment