Rais Kikwete ahudhuria Sherehe za Kusimikwa Wakfu Askofu Dkt. Alex Seif Mkumbo wa KKKT Dayosisi ya Kati, aanza ziara ya Siku nne ya Mkoa wa Tabora.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Askofu mpya wa KKKT Dayosisi ya kati Dkt
Alex Seif Mkumbo (mwenye fimbo) pamoja na viongozi wa kanisa hilo
wakiongozwa na Askofu Mkuu Dkt Alex Gehaz Malasusa (kulia kwa Rais),
Msaidizi mpya wa Dayosisi hiyo Mchungaji Syprian Yohana Hilinti (wa tatu
kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Kone na viongozi wengine katika
sherehe ya Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la
Singida Januari 6, 2013.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na kiongozi wa kanisa la KKKT
nchini Dkt Alex Gehaz Malasusa baada ya kupokea kamba kama ishara ya
kupokea zawadi ya ngombe toka kwa Dayosisi hiyo huku Askofu mpya wa
KKKT Dayosisi ya kati Dkt Alex Seif Mkumbo akishuhudia katika sherehe
ya Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida
Januari 6, 2013.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na kiongozi wa kanisa la KKKT
nchini Dkt. Alex Gehaz Malasusa na Askofu mpya wa KKKT Dayosisi ya
kati Dkt Alex Seif Mkumbo baada ya sherehe ya Kusimikwa Wakfu Askofu
Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida Januari 6, 2013.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ripoti ya mkoa wa Tabora toka kwa Mkuu
wa Mkoa Mhe Fatma Mwassa huo aliyosomewa mara baada ya kuwasili kuanza
ziara ya kikazi ya siku nne.(PICHA NA IKULU).
0 comments:
Post a Comment