Mahakama ya rufaa nchini Burundi imepunguza hukumu ya kifungo cha
maisha alichokuwa amehukumiwa mwandishi wa habari Hassan Ruvakuki na
kukifanya kuwa miaka mitatu gerezani.
Majaji wamesema kuwa, wamepunguza uzito wa mashtaka kutoka ugaidi hadi kuwa mwanachama wa genge.
Jaji wa Mahakama ya rufaa nchini Burundi, Fulgence Ruberintwari amesema kuwa, mwandishi habari huyo ana hatia ya kujihusisha na genge ambalo lilianzishwa kwa lengo la kuwashambulia watu na kuharibu mali.
Ruvakuki alikuwa akifanya kazi na radio moja ya kimataifa ya nchi moja ya Ulaya pamoja na vyombo vya habari ndani ya Burundi.
Mwezi Juni mwaka jana alikuwa amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani. Alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya kupanga njama ya mashambulizi ya silaha katika mkoa wa mashariki mwa Burundi wa Canzuko karibu na Tanzania.
CHANZO RADIO TEHRAN

0 comments:
Post a Comment