KUNDI
la wananchi wanaodaiwa kuwa na hasira, wamevamia kituo cha Polisi cha
Kibiti Wilayani Rufiji na kufanya vurugu kubwa baada ya raia mmoja kufa
kwa kile kilichodaiwa kipigo cha Polisi.
Chanzo
chetu cha Habari kutoka Kibiti kinaipasha kuwa kijana aliyefariki
kutokana na kipigo hicho ni Hamis Mpondi, ambaye mauti yamemfika wakati
akipatiwa matibabu Hospitali ya Muhimbili.
Habari
zaidi zinapasha kuwa hivi sasa wananchi hao wanaendelea kuteketeza
nyumba za Askari Polisi hao zilizopo jirani na kituo hicho, licha ya
Polisi kuendelea kufanya juhudi za kuwatawanya kwa mabomu katika eneo
hilo.
Aidha
wananchi hao wameanza kufunga barabara kuu ya Kilwa iendayo Mikoa ya
Kusini, Lindi na Mtwara kwa mawe, magogo na kuchoma matairi ikiwa ni
umbali wa kama kilometa moja kutoka kituo cha Polisi Kibiti.
Hali
inaelezwa kuwa inazidi kuwa tete huku Polisi wa Kibiti wakiendelea na
jitihada za kudhibiti hali hiyo kwa kufyatua mabomu hewani kujaribu
kutawanya umati huo wa watu. Vurugu zinaendelea, Habari kwa hisani ya
Father Kidevu.
0 comments:
Post a Comment