taka katika dampo lililo katika makazi ya watu maeneo ya kata ya kwa kilosa
taka mbele ya nyumba katika kata ya mivinjeni
mwandishi yahaya mohamedy wa ebony fm akimuhoji mwenyekiti wa kilabu cha pombe cha kijiweni
wanahabari katika ziara kwenye kilabu cha kijiweni manispaa ya iringa
hali mbaya ya uchafu katika madapo ndani ya manispaa ya iringa imegundulika baada ya wanahabari kufanya ziara ya kushtukiza katika kata mbili za mivinjeni na kwa kilosa zilizopo manispaa ya iringa.
wananchi katika maeneo hayo wamelalamika kutoondolewa kwa taka kwa muda mrefu hali inayohatarisha afya yao haswa kipindi hiki cha mvua.
aidha viongozi wa kata ya kwa kilosa hususani afisa mtendaji davis swebe amesema ukaguzi wa madampo hayo umeshafanyika ikiwa ni pamoja na kilabu cha pombe za kienyeji cha kijiweni kinachomilikiwa na manispaa na kinachosubiriwa ni utekelezaji wa malalamiko hayo.
hata hivyo amekiri upungufu na ubovu wa magari ya kuondolea taka ndio chanzo cha mlundikano wa uchafu huo.
0 comments:
Post a Comment