Main Menu

Tuesday, December 25, 2012

MANDELA ASHEREHEKEA X-MASS AKIWA NA AFYA NJEMA

                                            Rais wa zamani wa afrika kusini nelson mandela

Nelson Mandela,rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini akiwa hospitalini leo ametembelewa na mke wake Graca Machel na Rais Jacob Zuma.

Akizungumza katika siku hii ya Krismasi Zuma amesema wamemkuta Mandela katika hali ya uchangamfu na kwamba alikuwa na furaha kutembelewa katika sikukuu hii maalum,afya yake ilionekana kuwa nzuri zaidi na madaktari wana furaha na maendeleo ya afya yake. 

Kwa mujibu wa Zuma familia ya Mandela inathamini kwa dhati umma kuwa nao pamoja jambo ambalo linawapa nguvu hususan katika kipindi hiki kigumu.

Mandela mwenye umri wa miaka 94 ambaye ni alama ya kupinga utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini alilazwa hospitalini hapo tarehe nane mwezi wa Desemba ambapo aligunduliwa kuwa na maambukizi kwenye mapafu yake na baadae kufanyiwa upasuaji wa kuondowa vijiwe kwenye kibofu chake cha nyongo.

chanzo dw swahili

0 comments:

Post a Comment