Gor Mahia hawakufanya vizuri katika michuano
ya mwaka jana, ila wanatarajiwa kutoa ushindani katika mashindano ya mwaka huu.
Licha ya kupotea kwa
muda mrefu kabla ya kuibuka na kushindwa kufurukuta kwenye michauno ya mwaka
jana jijini Kigali, Gor Mahia wanajipa moyo Zaidi kutokana na mwenendo wao
kwenye Ligi ya Kenya.
Mabingwa hao wa Kenya hawajapoteza mechi
msimu huu huku wakionesha dalili za kutangaza ubingwa mapema kabisa.
KUNDI LAKE:
Gor Mahia iko kwenye
kundi A la michuano ya mwaka huu ikijumuishwa na Yanga, Al Khartoum ya
Sudan, KMKM ya Zanzibar na Telecom ya
Djibout. Ni kundi ambalo ni gumzo kuu likdaiwa kuwa na mechi zenye
msisimko Zaidi na ushindani mkubwa.
WACHEZAJI WA
KUANGALIWA:
Kwa wafuatiliaji wa soka nchini Kenya, hakuna
anayepinga kuwa kwa sasa timu yenye wachezaji bora zaidi ni Gor Mahia.
Wachezaji kama Khalid Aucho, chipukizi
Micheal Olunga anayetajwa kuwa mrithi wa mshambuliaji bora kuwahi kutokea
nchini Kenya, Dennis Oliech, na Meddie Kagere wamekuwa ni kiungo muhimu kwenye
timu hii.
Wachezaji wengine ni pamoja na mlinda mlango
Boniface Oluoch zake kutikiswa kwenye ligi ya Kenya inayoendelea kwa sasa.
Mlinzi wa Uganda Cranes, Godfrey Walusimbi na
George Odhiambo wakiongeza chachu kwenye timu hiyo.
BENCHI LA UFUNDI:
Gor Mahia inaongozwa na kocha Frank Nuttal,
raia wa Uskochi. Benchi lao la ufundi linajumuisha pia mlinda mlango wa zamani
wa kimataifa wa Harambe Stars, Mathew Ottamax ambaye ana jukumu la kuwanoa
walinda mlango, Boniface Oluoch na Jerim Onyango.
REKODI KOMBE LA
KAGAME:
Mara ya mwisho Gor Mahia ilitwaa ubingwa wa
Afrika Mashariki na Kati mwaka 1985, lakini imetwaa ubingwa huo mara 5 (1976,
1977, 1980, 1981, 1985).
0 comments:
Post a Comment