Mjumbe wa Kamati ya utendaji ya TFF na makamu
Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu nchini, Said Mohamed leo amefungua kozi ya
makocha wa golikipa inayoendelea katika ofisi za TFF zilizopo Karume.
Katika ufunguzi wa kozi hiyo, Said amesema
anashukuru FIFA kwa kuwapa nafasi ya kuendesha mafunzo hayo ya makocha wa
makipa kwa mara ya kwanza nchini, na kuwaomba washiriki wa kozi hiyo kutumia
nafasi hiyo vizuri kwa ajili ya kuendeleza mpira wa miguu nchini.
Jumla ya makocha 31 wanashiriki kozi hiyo
kutoka vilabu vyote viliyovopo Ligi Kuu na magolikipa wa zamani waliodakika
timu za Taifa.
Kozi hiyo ya makocha wa makipa inaendeshwa na
mkufunzi wa FIFA Elaxander kutoka nchini Ufaransa, ambapo kozi hiyo itafungwa
rasmi tarehe 17 Julai mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment