Mgombea urais kupitia chama cha mapinduzi CCM katika uchaguzi mkuu ujao utakao fanyika oct 25 JOHN POMBE MAGUFULI anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa michuano ya kombe la Kagame siku ya jumamosi uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Magufuli baada ya kufungua rasmi michuano
hiyo, atashuhudia mchezo wa ufunguzi rasmi wa mashindano ya Kagame, mechi
itakayowakutanisha miamba ya Afrika Mashariki timu ya Yanga dhidi ya Gor Mahia
kutoka nchini Kenya.
Michuano ya Kagame inatarajiwa kuanza kutimua
vumbi siku ya jumamosi kwa michezo mitatu, ukiondoa mechi ya Yanga Vs Gor
Mahia, mechi zingine zitakua ni kati ya APR dhidi ya Al Shandy uwanja wa Taifa
saa 8 mchana, KMKM Vs Telecom saa 10 jioni uwanja wa Karume.
Mchezo wa ufunguzi kati ya Yanga dhidi
ya Gor Mahia unaonekana kuteka hisia za wapenzi wa soka kwa ukanda wa Afrika
Mashariki, kwani ni takribani miaka 19 timu hizo mbili haziwaji kukutana katika
ardhi ya Tanzania.
Mara ya mwisho mwaka 1996 katika michuano ya
Cecafa, timu hizo zilikuwa katika kundi moja, katika mchezo wa awali zilitoka
sare ya bao 1- 1, wakati zilipokutana katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu,
Gor Mahia iliibuka na ushindi wa mabao 4 -0.
swali la msingi hapa ni kwamba klabu za Tanzania, Yanga, Azam na KMKM zitaweza kuhakikisha kombe
la michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki haliondoki kwenye ardhi yaTanzania?
0 comments:
Post a Comment