Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) itaanza Sept 12 badala ya Agosti 22 ili kumpa
Charles Mkwasa fursa ya kuendelea na program yake kuelekea mechi ya Taifa Stars
vs Nigeria itakayochezwa Sept 5.
Mechi ya Ngao ya Jamii (Community Shield)
itakayozikutanisha Azam FC dhidi ya Yanga SC sasa itachezwa Agosti 22 badala ya
Agosti 15.
Ratiba ya Ligi Kuu iliyokuwa imeandaliwa, sasa inafanyiwa
marekebisho kwa ajili ya tarehe mpya ya kuanza, ambapo pamoja na mambo mengine
mechi sasa zitachezwa wikiendi na katikati ya wiki na wikiendi ya Oct 25
hakutakuwa na mechi kupisha Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge.
Klabu za Ligi Kuu
zimeandikiwa barua kujulishwa tarehe mpya ya kuanza Ligi, na dirisha la usajili
linabaki kama lilivyo.
Wamiliki
wa viwanja vyenye upungufu wmeandikiwa barua kutakiwa kurekebisha upungufu
katika muda maalumu, vinginevyo havitaruhusiwa kutumika kwa ajili ya VPL na FDL.
Timu ya Madini ya Arusha imeruhusiwa kutumia Uwanja wa
Nyerere uliopo Mbulu mkoani Manyara kwa mechi za SDL kwa masharti upungufu
uliopo kwenye uwanja huo urekebishwe kwanza.
0 comments:
Post a Comment