Main Menu

Friday, May 22, 2015

JOSE MOURINHO KOCHA BORA WA MWAKA ENGLAND



Jose Mourinho's side have been No 1 in the Premier League since August 30 - a record 274 days at the top of the table so farTuzo zimezidi kumiminika katika klabu ya Chelsea baada ya kocha  wa timu hiyo Jose Mourinho kutangazwa kuwa kocha bora wa msimu wa Ligi Kuu ya soka nchini England.

Tuzo hiyo inaifuatia ile aliyotwaa mchezaji Eden Hazard ya kuwa mchezaji bora wa Ligi kuu ya soka nchini England msimu huu.

Jose Mourinho anatwaa tuzo hiyo baada ya kuiwezesha klabu hiyo ya darajani kuwa mabingwa wa Ligi Kuu ya soka nchini England baada ya kipindi cha takribani miaka mitano ya kutotwaa taji la Ligi Kuu.

Huu ni msimu wa pili kwa Mourinho kuifundisha klabu ya Chelsea baada ya kutimkia katika vilabu vya Inter Milan na Real Madrid  na msimu huu kurejea tena katika klabu ya Chelsea.

Katika kinyang’anyiro hicho cha kocha bora wa msimu wa Ligi ya England, Mourinho alikuwa akichuana na makocha wa timu nyingine kama Ronald Koeman (Southampton), Arsene Wenger (Arsenal), Gary Monk wa Swansea City na Nigel Pearson wa Leicester City.
 Mourinho with Eden Hazard, who won the Barclays Player of the Season award, during the recent draw at Arsenal
Hii ni mara ya tatu kwa kocha Jose Mourinho kuchukua tuzo ya kocha bora wa msimu kwani tayari alikwishachukua tuzo ya kocha bora wa msimu katika misimu ya 2004-05 na 2006-07 akiwa na klabu ya Chelsea.

Msimu uliopita kocha wa Crystal Palace Tony Pulis ndiye aliyekuwa kocha bora wa msimu baada ya kuiwezesha klabu hiyo kufanya vizuri na kubaki Ligi kuu ya soka nchini England.

PREVIOUS WINNERS 

Sir Alex Ferguson (11): 1993-94, 1995-96, 1996-97, 1998-99, 1999-2000, 2002-03, 2006-07, 2007-08, 2008-09, 2010-11, 2012-13
Arsene Wenger (3): 1997-98, 2001-02, 2003-04
Jose Mourinho (3): 2004-05, 2005-06, 2014-15
Kenny Dalglish (1): 1994-95
George Burley (1): 2000-01
Harry Redknapp (1): 2009-10
Alan Pardew (1): 2011-12
Tony Pulis (1): 2013-14


0 comments:

Post a Comment