Main Menu

Friday, May 22, 2015

PSG KUVUNJA BANK KUMNG'OA RONALDO REAL MADRID



Ronaldo is reportedly unhappy at the disproportion between his goals and club honours at the BernabeuKlabu ya PSG ipo tayari kutoa kiasi cha euro milioni 125 kwa ajili ya kupata saini ya mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo.

Hali ya klabu ya Real Madrid kwa sasa si shwari kutokana na timu hiyo kufanya vibaya msimu huu na hakuna matumaini ya benchi la ufundi la timu hiyo chini ya kocha Carlo Ancelooti kuwepo tena msimu ujao.

Cristiano Ronaldo amevunja rekodi nyingi msimu huu ikiwepo ya kuwa mfungaji bora wa pili wa klabu ya Real Madrid kwa kufikisha idadi ya magoli 310.

Rekodi hiyo imemfanya Ronaldo kubakisha magoli 13 tu kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu ya Real Madrid.

Kwa sasa nyota huyo anaongoza kwa ufungaji wa magoli katika Ligi Kuu ya soka nchini Hispania akiwa na magoli 45 huku mpinzani wake Messi akiwa na magoli 41.

0 comments:

Post a Comment