Main Menu

Friday, May 22, 2015

LIGI MBALIMBALI KUFIKIA TAMATI KESHO



Msimu wa Ligi mbalimbali unategemewa kumalizika hapo kesho ikiwa ni safari ya miezi takribani kumi ya ushindani katika Ligi hizo.

Ligi ambazo michezo yake inamalizika hapo kesho ni pamoja na Ligi ya Ujerumani Bundesliga, Ligi ya Hispania La Liga na Ligi ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1.

Ligi ya Ujerumani itamalizika kesho kwa michezo saba kupigwa katika viwanja saba tofauti.

Bingwa wa Ligi hiyo kishajulikana ambaye ni Bayern Munich lakini timu zipi zitashuka daraja bado ni kitendawili kinachohitaji kuteguliwa hapo kesho.

Timu za Paderborn na Hamburg SV zinaonekana zimeshashuka daraja kimahesabu ingawa michezo ya mwisho hapo kesho itaamua pia.

Lakini bado mustakabali wa timu nyingine ya tatu toka mkiani ambayo itacheza mtoano na timu iliyoshika nafasi ya tatu ya Ligi ya daraja la pili ya Bundesliga haijajulikana bado.

Timu za VFB Stuttgart,Hannover 96 na Freiburg zinapambana kutocheza hatua ya mtoano ya kubaki katika Ligi ya Bundesliga msimu ujao.
 
Nchini Ufaransa pia Ligi yao itamalizika siku ya kesho.
Tayari PSG ndio mabingwa wa Ligi ya Ufaransa kwa msimu huu ikiwa ni mara ya tatu mfululizo kwa PSG kuchukua Ligi Kuu ya Ufaransa maarufu kama French Ligue 1.

Mchezaji bora wa msimu huu kwa Ligi ya Ufaransa ni Alexandre Lacazette wa Olympique Lyon huku tuzo ya mchezaji bora chipukizi ikienda kwa Nabir Fekir wa Olympique Lyon pia na tuzo ya golikipa bora ikienda kwa Steve Mandanda wa Olympique Marseille.

Tuzo ya kocha bora wa msimu imeenda kwa kocha wa PSG Laurent Blanc.

Wakati Ligi za Ufaransa na Ujerumani zikifikia tamati hapo kesho,Ligi ya Hispania maarufu kama La liga  pia itafikia tamati hapo kesho pia.
Klabu ya Barcelona ndio mabingwa wa Hispania kwa msimu huu wa mwaka 2014/15.

Maswali ni  mengi ya nani atachukua tuzo ya mchezaji bora wa Ligi hiyo kwa msimu huu?Lakini vipi kwa  tuzo ya mfungaji bora wa Ligi hiyo (Pichichi) itaenda kwa Ronaldo au Messi?

Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo anaonekana kuwa katika nafasi nzuri ya kuwa mfungaji bora wa Ligi hiyo.

Kwa sasa Ronaldo ana magoli 45 akifuatiwa na Messi mwenye magoli 41.Tusubiri michezo ya mwisho ya La Liga hapo kesho
 Protest group AshleyOut.com are planning further demonstrations for the final day of the season
Ligi Kuu ya soka nchini England yenyewe itafikia tamati siku ya Jumapili huku Ligi ya Italia ikisogea kwa juma moja mbele ili kumalizika.

0 comments:

Post a Comment