Main Menu

Monday, May 25, 2015

BAKARI SHIME KUTUA AFRICAN SPORTS



 
Katika kuboresha kikosi na benchi la ufundi la timu iliyopanda ligi kuu msimu ujao African Sports, uongozi wa timu hiyo upo katika mipango ya kumuajiri kocha wa Mgambo Shooting Bakari Shime.

Meneja wa kocha huyo ajulikanae kama mchawi mweusi Martin Kibua amesema tayari wameshapata ofa mbalimbali ikiwemo ya timu yake ya sasa ya mgambo na timu ya African Sports.

Mkataba wa Shime na mgambo shooting unamalizika mwishoni mwa mwezi huu.

Kuhusu mustakabali wa wapi atafanya kazi msimu ujao shime amesema hiyo ni kazi ya wakala na meneja wake yeye kazi yake ni kufundisha mpira tu.

Aidha Shime amesisitiza yupo tayari kufundisha timu yoyote pasipo kujalisha ni ya taasisi au wanachama kwa sabuba ili ufanikiwe ni lazima uzishinde changamoto.

African Sports ni miongoni mwa timu 4 zilizopanda ligi kuu kwa ajili ya msimu ujao baada ya kuwa nje ya ligi kuu kwa miaka 23.

0 comments:

Post a Comment