Leo jumapili tarehe 24, Mei 2015
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF imeketi katika
ukumbi uliopo makao makuu ya Shirikisho uwanja wa Karume.
Kamati ya Utendaji imepitia masuala
mbalimbali na kutoa maamuzi yafuatayo:
CLUB LICENCING (Leseni za vilabu)
Kamati ya Utendaji imeiagiza sekretarieti ivisisitize vilabu vya Ligi Kuu umuhimu wa kukamilisha maombi yao ya ushiriki wa ligi kuu kwa msimu wa 2015/16 kwa kuwasilisha fomu za maombi ya Leseni za vilabu TFF. Klabu ambayo haitakamilisha mchakato huo haitaruhusiwa kushiriki ligi kuu ifikapo msimu wa 2015/16.
Kamati ya Utendaji imeiagiza sekretarieti ivisisitize vilabu vya Ligi Kuu umuhimu wa kukamilisha maombi yao ya ushiriki wa ligi kuu kwa msimu wa 2015/16 kwa kuwasilisha fomu za maombi ya Leseni za vilabu TFF. Klabu ambayo haitakamilisha mchakato huo haitaruhusiwa kushiriki ligi kuu ifikapo msimu wa 2015/16.
KOMPYUTA - Kutokana na maamuzi ya
mkutano mkuu wa TFF uliofanyika Morogoro ambao uliagiza wanachama wake wapya
wapewe kompyuta, agizo hilo limetekelezwa na kompyuta hizo watakabidhiwa
wajumbe wa Kamati ya Utendaji wanaotoka kanda hizo ili waziwakilishe maeneo
husika. Mikoa hiyo ni Geita, Katavi, Manyara, Njombe na Simiyu.
MFUKO WA FDF - Kufuatia mkutano mkuu
wa TFF kuingiza kipengele cha FDF katika katiba yake, kikao cha Kamati ya
Utendaji wa mujibu wa katiba kimepitisha kanuni za uendeshaji wa mfuko huo.
Aidha kikao
hicho kimeteua wajumbe wafuatao wawe wajumbe wa
tume hiyo
(i)Tido Mhando -
Mwenyekiti,
(ii) Deogratius
Lyatto - Makamu mwenyekiti
(iii)Ephraim
Mafuru - mjumbe,
(iv)Beatrice
Singano - mjumbe,
(v)Joseph Kahama
- mjumbe
(vi)Ayoub
Chamshana - mjumbe.
Pia Henry Tandau ameteuliwa kuwa
katibu mtendaji wa mfuko huo.
AJIRA
Kamati ya Utendaji ya TFF imemteua
Boniface Wambura kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Bodi ya Ligi Kuu nchini
kuanzia tarehe 01, Juni 2015.
Wambura kabla ya uteuzi huo alikua
mkurugenzi wa mashandano TFF.
TFF inampongeza Wambura kwa uteuzi
na inaamini atatoa mchango mzuri katika kukuza na kuzitangaza ligi zetu.
Kamati ya utendaji imemteau Martin
Chacha (mratibu wa timu za Taifa) kukaimu nafasi ya mkurugenzi wa mashandano
TFF.
TIMU ZA TAIFA
Kamati ya utendaji ya TFF
imesikitishwa na mwenendo mbovu wa Taifa Stars Rais wa TFF, Jamal Malinzi kwa
niaba ya kamati ya utendaji amewaomba radhi wapenzi wa mpira kwa matokeo mabaya
ya Taifa Stars kwenye michuano ya Cosafa.
Kikao cha kamati ya utendaji
kilipokea taarifa juu ya mwenendo wa timu ya Taifa.
Baada ya majadiliano ya kina,
ilikubaliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa, Mart Nooij apewe changamoto
maalumu ya kufuzu kwa fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN na
asipofanikisha jambo hilo mkataba wake utasitishwa mara moja.
Maamuzi haya yamezingatia hali
halisi ya timu ya Taifa ambayo inakabiliwa na michuano mbalimbali ya kimataifa
ndani ya kipindi kifupi.
Aidha katika kuliimarisha benchi la
ufundi la timu ya Taifa, Leopald Tasso Mkebezi ameteuliwa kuwa meneja mpya wa
timu ya Taifa.
Mkebezi amewahi kuwa meneja wa timu
ya Taifa katika kipindi cha mwaka 2006 - 2012.
0 comments:
Post a Comment