Main Menu

Tuesday, April 21, 2015

NDUMBARO VS TFF MEI 10



Kamati ya Rufaa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF iliyokutana Aprili 19, 2015 imepanga kusikilizwa kwa rufaa ya Damas Ndumbaro Mei 10 mwaka huu, makubaliano ambayo yalifikiwa na pande zote mbili kwa pamoja.

Kikao hicho  kilipitisha taratibu za kisheria ambazo zitatumika kuamua kesi hiyo, ambazo ni taratibu kama zinazotumika mahakamani ikiwemo kuwasilisha  hoja kwa mdomo na si maandishi, kitendo ambacho kimekubaliwa na pande zote mbili.

Utaratibu huu umekua ukitumika katika mahakama za kawaida kuepusha manung'uniko kwa upande mmoja kulalamika umeonewa.

0 comments:

Post a Comment