Main Menu

Wednesday, April 22, 2015

BAYERN YAWASHANGAZA PORTO, ATLETICO,REAL KUMALIZANA LEO

Bayern Munich celebrate in front of their delighted fans after overturning a first leg deficit to reach the Champions League semi-finalsTimu za Bayern Munich ya Ujerumani na Barcelona ya Uhispania zimefanikiwa kusonga mbele kwa kutinga nusu fainali mashindano ya Klabu Bingwa Barani  Ulaya baada ya kushinda mechi zao hapo jana usiku. 

Baada ya kuchezea kichapo cha cha bao 3-1 katika mechi ya awali dhidi ya FC Porto  ya Ureno ugenini, hatimaye Bayern Munic waliigeuzia kibao Porto na kuirarua bila huruma mabao 6-1 na hivyo kuwa na njia nyeupe ya kutinga nusu fainali kwa ushindi wa jumla ya magoli 7-4. 
 Lewandowski slides on his knees in front of the Allianz Arena crowd after scoring his second goal of the night as Bayern raced away
Nao Barcelona baada ya ushindi wa awali wa bao 3-1 dhidi ya PSG mjini Paris, hapo jana imeendeleza vipigo dhidi ya Wafaransa hao baada ya kuwakandamiza kwa mabao bao 2-0, yaliyotiwa wavuni na Mbrazil Neymar katika kipindi cha kwanza. 
 Neymar (top) celebrates with Brazilian compatriot Dani Alves after scoring his and Barcelona's second goal of the night
Kwa matokeo hayo Barcelona imefuzu nusu fainali kwa ushindi wa jumla ya magoli 5-1. 
 
Mechi nyingine za robo fainali zinakamilika hii leo, pale Juventus ya Italia itakaposhuka uwanjani kumenyana na AS Monaco ya Ufaransa, huku shughuli nyingine pevu ikitarajiwa kuonekana kwenye dimba la Santiago Bernabeu, pale mabingwa watetezi Real Madrid watakapo wakaribisha watani wao wa jadi Atletico Madrid. 
Ancelotti watches his players during the training session ahead of the crucial Champions League tie
Katika mechi ya awali mafahali hao wawili walitoka suluhu ya bila kufungana.

0 comments:

Post a Comment