Main Menu

Friday, July 19, 2013

RIHANNA AMWAGIWA CHIPS JUKWAANI BAADA YA KUCHELEWA KWENYE SHOW…


All change: A blonde Rihanna leaving the Lowry Hotel in Manchester on Tuesday
Inavyoonekana mashabiki wa Rihanna wameanza kuchoshwa na tabia yake ya uswahili wa kuchelewa kwenye maonesho yake, na safari hii baadhi walimuandalia dawa yake kwa kuamua kumwagia chips jukwaani baada ya kuchelewa kufika katika onesho lake la Diamonds huko Manchester, Uingereza.

Japo akili ya mwimbaji huyo wa Diamonds haikujiongeza haraka kuutumia ule mwamvuli wake maarufu ‘Umbrella’ kujikinga na chips hizo kutoka kwa mashabiki hao ambao pamoja na hasira lakini bado walimngojea kwa hamu.

Rihanna (25) alichelewa kwa saa moja tu, lakini hii si mara ya kwanza kuchelewa katika matamasha yake na kuwafanya mashabiki waliofika kwa wingi kumwona wapandwe na gadhabu. 

Mwezi (march) mwaka huu alichelewa masaa 2 katika onesho lake la Montreal, Canada na (July 6) akiwa amelewa chakali alichelewa tena masaa mawili katika show yake ya Poland.

Mrembo huyo wa Barbados baada ya kupokea zawadi hiyo (chips) kutoka kwa mashabiki wenye gadhabu akiwa jukwaani alijibu mashambulizi hayo kwa maneno makali “There’s a good crazy and there’s a bad crazy. 

When you throw s*** up here, that’s an epic fail.  I wanna get your gifts but I don’t want you to knock my people out”.

0 comments:

Post a Comment