Main Menu

Monday, September 1, 2014

FALCAO ATUA MAN UNITED KWA MKOPO WA MUDA MREFU

KLABU ya Manchester United imeshinda mbio za kuwania saini ya mshambuliaji Radamel Falcao kutoka Monaco kwa mkopo wa mwaka mmoja.
Mshambuliaji huyo ataigharimu klabu hiyo  Pauni Milioni 12 kwenda kuungana na Angel di Maria, Daley Blind, Luke Shaw, Ander Herrera na Marcos Rojo katika orodha ya wachezaji wapya kwenye kikosi cha Louis van Gaal.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Colombia mwenye umri wa miaka 28 tayari ameafiki kulipwa mshahara wa Pauni 200,000 kwa wiki na anatarajiwa kutua Manchester wakati wowote kwa ndege binafasi kukamilisha taratibu.
Kimeeleweka: Manchester United imemnasa Radamel Falcao kwa mkopo kutoka Monaco

REKODI YA FALCAO...

River Plate (2005-2009): Mechi 105 mabao 45
Porto (2009-2012): Mechi 87 mabao 72
Atletico Madrid (2011-2013): Mechi 91 mabao 70
Monaco (2013-2014): Mechi 22 mabao 13
Colombia: Mechi 51 mabao 20

0 comments:

Post a Comment