Main Menu

Monday, September 1, 2014

CHICHARITO HUYOOO MADRID KWA MKOPO

Mshambuliaji wa kimataifa wa Mexico Javier Hernandez amekamilisha uhamisho wake wa mkopo kwenda Real Madrid pamoja na uwezekano wa kununuliwa moja kwa moja kutoka Manchester United baadaye.
 
Real inamchukua mchezaji huyo baada ya kufaulu vipimo vya afya leo mjini Madrid.
 
United inataka dau la Pauni Milioni 17 kumuuza moja kwa moja mchezaji huyo, lakini kwa mkataba wa sasa wa mkopo wa muda mrefu wa msimu, Louis van Gaal anachukua Pauni Milioni 1.5.
 
United imethibitisha katika ukurasa wake wa Twitter leo kumtoa kwa mkopo mchezaji huyo kwenda Real Madrid. 

0 comments:

Post a Comment