Main Menu

Wednesday, July 24, 2013

LIVERPOOL YAIPIGA TENA CHINI OFA YA ARSENAL YA PAUNDI MILIONI 40 KWA AJILI YA SUAREZ



Klabu ya liverpool  inayoshiriki ligi kuu ya England imekataa ofa mpya ya paundi milioni 40 kutoka timu ya Arsenal Kutaka kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay Luis Suarez. 


Hii ni ofa ya pili kwa klabu Arsenal kukataliwa na Liverpool kwa kipindi kisichozidi wiki tatu kwa mchezaji huyomwenye umri wa miaka 26 ambaye alifunga magoli 30 kwenye mechi 44 alizocheza msimu uliopita.


Haijajulikana Liverpool inahitaji kiasi gani iliwakubali ofa ya washika bunduki hao wa jiji la London ambao wameshikilia msimamo wa kutaka kumsajili mshambuliaji ambaye ameifungia klabu yake magoli 51 kwenye mechi 96 za mashindano yote.


Kama Arsenal watatuma ofa itakayozidi paundi milioni 50 huenda ikakubaliwa kutokana kauli ya kocha wa Liverpool  Brendan Rodgers kufananisha dau la uhamisho la paundi milioni 55 wa Edinson Cavani kwenda PSG ndio thamani halisi ya luis suarez .

0 comments:

Post a Comment