Main Menu

Wednesday, July 24, 2013

JOSE MOURINHO AIPA UBINGWA WA EPL MANCHESTER CITY



Kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho ameipa nafasi kubwa timu ya Manchester city kufanya vizuri na hata kuchukua taji la ligi kuu nchini England kutokana na kufanya usajili mzuri pia wana meneja mzuri.


Wametumia zaidi ya paundi milioni 90 kufanya usajili wa wachezaji mahiri na wazoefu wanne pia kocha raia wa Chile  Manuele Pelegrini ambaye pia msimu uliopita alifikisha klabu ya Malaga  nusu fainali ligi ya mabingwa wa ulaya.


Wachezaji hawa wataongeza ubora kwenye kikosi cha Manchester City na kuongeza ushindani na wataleta utofauti kati ya wao waliosajili wachezaji bora na timu ambazo hazijafanya usajili .


Manchester city imewasajili Fernandinho kutoka Shakhtar Donetsk, Jesus Navas, Alvaro Negredo kutoka Sevilla na kiungo mshambuliaji  wakimataifa  wa Montenegro  Stevan Jovetic,kutoka klabu ya Fiorentina.

na issa maenda wa ebony fm

0 comments:

Post a Comment