Main Menu

Wednesday, July 24, 2013

JUVENTUS YA ITALIA YAONGOZA KWA KUPATA MAPATO MAKUBWA KATIKA MICHUANO YA ULAYA MSIMU ULIOPITA

Shirikisho la kandanda barani Ulaya, UEFA, limetangaza mapato ya vilabu mbalimbali katika msimu uliopita wa michuano ya Kombe la Mabingwa wa Ulaya, Champions League, na Kombe la Ligi la Ulaya, Europa League. 


Timu iliyojipatia mapato zaidi kutokana na michuano hiyo ni Juventus ya Italia, ambayo imepata Euro milioni 65. 


Timu ya Bayern Munich ya Ujerumani, imejipatia Euro milioni 55, huku timu ya Chelsea ya Uingereza, ikiwa imepata zaidi ya Euro milioni 10.

0 comments:

Post a Comment