
Taarifa zinasema kuwa, sheria hiyo imepitishwa na kamisheni ya familia nchini humo.
Kamisheni hiyo imeeleza kuwa sheria ya ukomo wa kuzaa watoto wawili tu imewekewa Waislamu tu na kwamba Mabudha wanaruhusiwa kuzaa zaidi ya idadi hiyo.
Makundi ya kutetea haki za binadamu yamekosoa vikali sheria hiyo na kusema kuwa inakiuka wazi haki za binadamu.
Waislamu wa Myanmar wanakabiliwa na hali ngumu ikiwa ni pamoja na kuchomwa moto nyumba zao, kunyanyaswa, kudhalilishwa na hata kuuawa, vitendo vinavyofanywa na Mabudda wenye misimamo ya kufurutu mipaka.
Chanzo radio tehran
0 comments:
Post a Comment