Idadi ya watuhumiwa katika kesi inayomkabili mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa imefikia 92 baada ya watuhumiwa wengine 11 kufikishwa mahakamani leo.
Akisoma mashtaka mbele ya hakimu mkazi salome kayombo, Mwendesha mashtaka wa serikali Kasana Maziku ameieleza mahakama kuwa washtakiwa hao wameongezwa katika kesi inayomkabili Mchungaji Peter Msigwa.
Maziku amesema washtakiwa hao wanakabiliwa na kosa la pili katika kesi hiyo ambalo ni kufanya maandamano bila kibali na kinyume na sheria, na kosa la tatu la kuharibu mali kwa makusudi.
Maziku amesema watuhumiwa hao wametenda makosa hayo tarehe 19 mwezi wa tano mwaka huu katika eneo la mashine tatu manispaa ya Iringa.
Katika kesi hiyo mchungaji Peter Msigwa mbali ya kukabiliwa na kosa la pili na tatu pia anakabiliwa na kosa la
kwanza la kuhamasisha watu kutenda ualifu.
Hata hivyo kati ya watuhumiwa hao kumi na moja, Kumi kati yao wameachiwa kwa dhamana na mshtakiwa mmoja amerudishwa mahabusu kutokana na kukosa mdhamini.
Kesi hiyo imetajwa kusikilizwa tena tarehe tatu mwezi wa sita mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment