·Baada ya Mshindi
wa Mahela kuzoa Milioni 100 Sasa ni Cheka Nao.
·Maelfu ya Watanzania
kucheka na mamilioni
Siku chache baada ya Mwanafunzi
wa chuo cha ualimu Kasulu mkoani Kigoma, Valerian Nickodemus (22) kuibuka
kidedea na kujishindia kitita cha Shilingi milioni 100 katika promosheni ya
MAHELA iliyoendeshwa kwa mafanikio makubwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom
Tanzania, sasa ni zamu ya Watanzania wengine kujumuika na kucheka nae baada ya
kuzinduliwa tena kwa Promosheni nyingine ya Cheka Nao.
Promosheni
hiyo ambayo imezinduliwa hivi karibuni itaendelea kuleta faraja na mafanikio
kwa wateja wa kampuni hiyo kwa kuweza kujinasua katika hali duni ya maisha.
Baada
ya zaidi ya Watanzania 300 kunufaika kwa kujishindia fedha taslimu katika
Promosheni ya MAHELA iliyomahitimishwa Aprili 24 mwaka huu, sasa zaidi ya
wateja 6000 wa Vodacom watajishindia Zawadi mbali mbali kwa kipindi cha siku
60.
Akizungumza
wakati akikabidhiwa fedha zake za Ushindi, mshindi wa Shilingi Milioni 100 wa
Promosheni ya MAHELA, Valerian Nickodemus amewaomba Watanzania kutambua mchango
mkubwa unaofanywa na Kampuni ya Vodacom nchini katika kujenga na kuimarisha
maisha ya Watanzania.
Nae
Mkuu wa kitengo cha masokona mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa amesema kuwa
kampuni yake itaendelea kuboresha maisha ya Watanzania kupitia njia mbalimbali
na kuwasihi sasa wateja wa kampuni hiyo kujitokeza kushiriki promosheni mpya ya
Cheka nao.
Pamoja
na mambo mengine benki ya NMB imejitolea kutoa mafunzo ya ujasiriamali na
matumizi sahihi ya fedha kwa Mshindi huyo ili kumuwezesha kuwa na matumizi
yenye tija.
Akizungumza
katika hafla hiyo iliyofanyika katika makao makuu ya benki ya NMB, Mkuu wa
Kitengo cha Wateja Binafsi Abdulmajid Nsekela, amesema kuwa benki yake imekuwa
na ushirikiano mzuri wa kibiashara na kampuni ya Vodacom hasa kupitia huduma
yake ya M - pesa.
Promosheni
ya Cheka Nao inatoa fursa kwa Wateja wa mtandao wa Vodacom kujiunga na huduma
ya Cheka Nao kwa kupiga *149*01# ambapo mteja atapata dakika 20 za kupiga
kwenda mitandao yote zinazotozwa kwa sekunde, SMS 150 na MB 60 zinazotumika kwa
masaa 24 na kupata nafasi ya kujishindia fedha taslim ambapo zaidi ya shilingi
Milioni 200 zimetengwa kwa ajili ya zawadi kwa washindi. Washindi 10
watajishindia shilingi 50,000/- kwa siku, washindi wengine 100 watajishindia
shilingi 10,000/- kwa siku na washindi watano watajishindia shilingi 2m/- kwa
mwezi.
0 comments:
Post a Comment