Serikali ya Australia imetengua baadhi ya vikwazo ilivyoviweka dhidi ya
baadhi ya viongozi wa Zimbabwe.
Bob Carr Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje
wa Australia amesema kuwa, serikali ya nchi hiyo imefuta vikwazo
ilivyoviweka dhidi ya viongozi 65 wa Zimbabwe wakiwemo viongozi wa ngazi
za juu wa serikali na wa kijeshi wa nchi hiyo.
Bob Carr ameongeza kuwa,
hatua hiyo imechukuliwa baada ya serikali ya Harare kukamilisha zoezi
la uundwaji wa katiba mpya, ambayo ni chachu ya kufanyika mabadiliko
kwenye muundo wa utawala nchini humo.
Inafaa kuashiria hapa kuwa,
wajumbe wa Bunge la Seneti la Zimbabwe tarehe 14 Mei waliipitisha rasimu
ya katiba mpya na kutiwa saini baadaye na Rais Robert Mugabe tarehe 22.
Radio Tehran Kiswahili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment