Main Menu

Monday, May 27, 2013

NDOA YA JINSIA MOJA YAZIDI KUPINGWA NCHINI UFARANSA


Takriban watu 100 wamekamatwa wakati wa maandamano ya kupinga ndoa ya jinsia moja mjini Paris. 

Watu 150,000 waliandamana katika mji mkuu huo wa Ufaransa hapo jana katika maandamano makubwa yaliogeuka ghasia kupinga muswada wa ndoa za jinsia moja uliotiwa saini kuwa sheria na Rais Francois Hollande wiki iliyopita kufuatia mjadala mkali wa miezi kadhaa juu ya suala hilo.

Maandamano yalianzia katika sehemu mbalimbali na kuishia katika eneo la Invalides katikati ya jiji. 

Waandamanaji walikuwa wakitaka kutenguliwa kwa sheria hiyo kwa kusisitiza umuhimu wa familia na haki ya mtoto kwa familia. 

Polisi ilitumia mabomu ya kutowa machozi wakati wa mapambano na wafuasi wa sera kali za mrengo wa kulia ambao pia walikuwepo katika maandamano hayo.

0 comments:

Post a Comment