Ligi
ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) kuwania nafasi tatu za kucheza Ligi Daraja
la Kwanza (FDL) msimu ujao inaingia raundi ya pili wikiendi hii kwa
kukutanisha timu 14 zilizofanikiwa kusonga mbele.
Timu
zitakazocheza raundi hiyo kwa mtindo wa nyumbani na ugenini ni Abajalo
ya Dar es Salaam itakayokuwa mwenyeji Kariakoo ya Lindi katika mechi
itakayochezwa Jumamosi (Mei 25 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume.
Siku
hiyo hiyo Uwanja wa Azam ulioko Chamazi utatumika kwa mechi kati ya
Friends Rangers ya Dar es Salaam na African Sports ya Tanga wakati
Jumapili (Mei 26 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Machava FC ya
Kilimanjaro na Mpwapwa Stars ya Dodoma itakayochezwa Uwanja wa Ushirika
mjini Moshi.
Stand
United ya Shinyanga itakuwa mgeni wa Magic Pressure ya Singida katika
mechi itakayochezwa Jumapili (Mei 26 mwaka huu) Uwanja wa Namfua mjini
Singida wakati Polisi Jamii ya Mara na Biharamulo FC ya Kagera zitaumana
siku hiyo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.
Mjini
Kigoma kutakuwa na mechi kati ya wenyeji Saigon FC na Katavi Warriors
ya Katavi. Nayo Kimondo SC ya Mbeya itakuwa mgeni wa Njombe Mji ya
Njombe katika mechi itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Sabasaba.
Mechi
za marudiano zitachezwa kati ya Juni 1 na 2 mwaka huu wakati timu
zitakazofuzu kucheza raundi ya tatu zitacheza mechi za kwanza kati ya
Juni 8 na 9 mwaka huu wakati mechi za marudiano zitakuwa kati ya Juni 15
na 16 mwaka huu.
LIUNDA KUTATHMINI WAAMUZI MECHI YA FIFA
Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limemteua Leslie Liunda wa
Tanzania kuwa mtathmini wa waamuzi (referee assessor) katika mechi ya
mchujo ya Kombe la Dunia.
Mechi
hiyo ya Kundi B, Kanda ya Afrika kati ya Cape Verde na Equatorial
Guinea itafanyika Juni 8 mwaka huu saa 10.30 jioni kwenye Uwanja wa
Verzea mjini Praia.
Waamuzi
wa mechi hiyo ambao watatoka Angola ni Martins De Carvalho Helder, Dos
Santos Jerson Emiliano, Da Silva Lemos Julio na Muachihuissa Caxala
Antonio. Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Diarra Massa Momoye wa
Mauritania.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment