Main Menu

Wednesday, May 22, 2013

WAFANYABIASHARA WA MANISPAA YA IRINGA WATAKIWA KUWA WATULIVU WAKATI MAPENDEKEZO YAO YANAFANYIWA KAZI NA MANISPAA


                  mstahiki meya wa manispaa ya iringa aman mwamwindi

Siku tatu baada ya kutokea kwa vurugu kati ya wafanyabiashara na polisi manispaa ya iringa, Mstahiki meya wa manispaa hiyo amewataka wafanyabiashara hao kuwa watulivu wakati mapendekezo yao yanafanyiwa kazi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, mstahiki meya wa manispaa ya Iringa Aman Mwamwindi, amesema kuwa baraza la madiwani limesikitishwa na tukio la jumapili.

Mwamwindi amesema mapendekezo yote ya wafanyabiashara waliyoyatoa walipofanya kikao na mkurugenzi wa manispaa tarehe 9 mwezi huu yatajadiliwa tarehe 28 mwezi huu na kamati ya fedha na uongozi kwa niaba ya baraza.
 

 
Aidha Mwamwindi amewasihi wafanyabiashara kuendelea kufanya biashara zao katika eneo la Mlandege hadi manispaa hiyo itakapokutana na kutoa maamuzi.
 


Kuhusiana na lawama zinazoelekezwa kwake kuwa kauchukulia mgogoro huo kisiasa, Mwamwindi amesema mgogoro huo haupo kiitikadi
na amemtaka mbunge wa jimbo la iringa mjini mchungaji peter msigwa kuhudhuria kikao hicho ili kufikia maamuzi.

                           mkuu wa mkoa wa iringa dr christine ishengoma
 
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma, amesema mkoa wa iringa hauna kawaida ya vurugu na amewataka wananchi wasiyumbishwe na vyama vya siasa.
 

0 comments:

Post a Comment