mchungaji peter msigwa akifikishwa mahakamani mchana wa leo mkoani iringa
mchungaji msigwa akiteta na wakili wa kujitegemea bazili mkwata mahakamani hapo
wafuasi wa chadema wakitoka mahakamani baada ya mbunge wa iringa mjini kuachiwa kwa dhamana
kundi kubwa la wafuasi wa chadema wakiandamana kuelekea ofisi za chama hicho wilaya kwa ajili ya kumsikiliza mbunge wao aliyeachiwa kwa dhamana
msigwa akiwa amebebwa juju na wafuasi wake
mbunge huyo amebebwa juu juu kwa umbali wa zaidi ya kilometa moja baada ya kuachiwa kwa dhamana
wafuasi wa chadema wakimsikiliza mchungaji peter msigwa nje ya ofisi za wilaya za chama hicho mkoani iringa
msigwa akizungumza na wafuasi wake
Wananchi wa manispaa ya iringa wametakiwa kuwa
watulivu baada ya mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA)
kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kushawishi watu kutenda uhalifu.
Akizungumza na wafuasi wa Chadema katika ofisi za
wilaya za chama hicho mkoa wa Iringa mara baada ya kuachiwa kwa dhamana, Msigwa
amewataka wafuasi hao na wananchi kwa ujumla kuwa watulivu na kuiachia kazi
mahakama ambayo wana imani nayo.
Aidha Msigwa amewashukuru wananchi na wanachama wa
chadema kwa ushirikiano waliouonyesha na kufanikisha kupata dhamana kwa watu waliokamatwa huku wengine wakitarajiwa
kuwekewa dhamana leo
Wakizungumza na mtandao huu baadhi ya wananchi
wameishauri serikali kukaa na wananchi hao badala ya kutumia jeshi la polisi
kutatua mgogoro kati yao.
Msigwa na watuhumiwa wengine 66 wamefikishwa
mahakamana wakikabiliwa na mashtaka matatu tofauti kutokana na vurugu
zilizotokea manispaa ya Iringa siku ya tarehe 19 mwezi huu.
Watuhumiwa hao wanakabiliwa na tuhuma za kushawishi
watu kutenda ualifu shtaka linalomkabili mchungaji msigwa, kukusanyika bila
kuwa na kibali na kuharibu mali kwa makusudi.
Katika kesi hiyo iliyotajwa kusikilizwa tena tarehe
3 mwezi wa sita kutokana na upelelezi kutokamilika, Watuhumiwa 40 kati ya 67
wameachiwa kwa dhamana huku wengine 27 wakirudishwa mahabusu.
0 comments:
Post a Comment